UTAYATAMBUAJE MAYAI YANAYOFAA KUTOTOLESHA
Vigezo vya uchaguzi wa mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kutotoleshwa Si kila yai linalotagwa na kuku basi linakidhi sifa na vigezo vya kutotoleshwa ni wazi kuwa kama yai halikidhi vigezo vya kutotoleshwa na kuwa kifaranga hata uwezekano wa kutototoleshwa wenyewe unakuwa haupo. Wafugaji wengi tumekuwa tukikusanya mayai hovyo hovyo na kuyapelekwa kutotoleshwa bila kuzingatia vigezo hivi muhimu;- 1. A) YAWE YAMERUTUBISHWA NA JOGOO Sifa kuu na muhimu ya utotoleshwaji wa mayai ni kuwa ni lazima yawe yamerutubishwa na jogoo kwa uwiano stahili wa majogoo na mitetea na uwiano unaopendekekzwa ni wa mitetea nane kwa jogoo mmoja. 2.YAWE NA GANDA SAFI LISILO NA UFA Mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kutotoleshwa ni lazima yawe na ganda safi lisilo na uchafu uliogandia.Usafi wa mayai unategemea pia na usafi wa bandani na mahali ambapo kuku wanatagia. Iwapo kuku watakua na miguu misafi na wanataga kwenye viota visafi na ukusanyaji wa mayai unafanywa kwa wakati na kuwekwa kwenye chombo kisafi ni wa...