KILIMO CHA WHATSAPP
Najua unashahuku kweli kufahamu ni Kilimo gani naongelea.Nadhani unajua kwamba kupanga ni kuchagua hivyo kama umepanga kujikita kwenye kilimo Jua kabisa umeshachagua na kukubali matokeo.
Leo tunakukumbusha hasa kwa wale wanaolima huku wanajipa matumaini kwa kutumia mitandao ya kijamii kama whatsaap..
Hapa tunachoongelea hasa ni kutohudhuria shambani kwako na kupata maendeleo ya shamba kwa kutumia whatsaap.
Ndugu yangu wengi wamelia kwenye Kilimo cha hivyo jitahidi sana kutembelea shamba lako usije ukavuna mabua.
Kilimo kinahitaji kujitoa, uvumilivu pia na kutumia akili ńyingi.
Tunakuomba sana ili kupata mazao bora ni vyema na wewe Mmiliki uwe unahudhuria shambani kwako.
Asante

Comments
Post a Comment