Posts

KILIMO CHA KABICHI

Image
KILIMO CHA KABICHI  Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa(cauliflower),kibichi kichina na kale.  MIZIZI  mizizi ya kabichi hutawanyika ardhin vizuri kwa kawaida huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 CM) na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano(75CM)  SHINA  Shina La mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au Zambarau.Hii hutegemeana na aina ya kabichi na kwa kawaida ni fupi.  HALI YA HEWA  Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi.Joto Jingi pia husababisha kulegea kwa kichwa vilivyofunga.Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari  UDONGO  Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huwo usiwe na chumvi chumvi nying na usiotuamisha maji.Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo ...

JINSI YA KUTUNZA VIFARANGA WIKI 1-5

Image
Kuku ni ndege wafugwao na binadamu wengi kwa ajili ya matumizi mbalaimbali ya binadamu. Mara nyingi hutumika kwa ajili ya kitoweo na kwa biashara pia. Wafugaji wengi hupenda kufuga kuku maana ni mwepesi kumtunza na hana garama kubwa za utunzaji ukilinganisha na wanyama wengine wafugwao. leo tutaangali jinsi ya kuwalea vifaranga had wafae kuwa kuku wakubwa;  Nyumba ya vifaranga;  nyumba ya vifaranga inatakiwa kuwa karibu na nyumba ya kuishi ili uweze kuwaangalia vifaranga kwa ukaribu zaidi, ijengwe kwenye sehemu iliyotulia kulingana na mwelekeo wa upepo na kuta zisiingize baridi sana pia iwe na eneo la kutosha kulelea vifaranga.  mfano wa nyumba ya vifaranga iliyotengenezwa na mfugaji mwenyewe  nyumba hiyo imejegwa maalumu kwa ajilinya kutunzia vifaranga katika ustadi mzuri kabisa.  Baadhi ya wafugaji hutengeneza nyumba za kufugi ilimradi katengeneza bila kutumia vipimo au ufanisi mzuri ili kulea vifanganga vizuri.  mfano wa nyumba ya vifaranga a...

SABABU ZA KASUKU/CHIRIKU🐦 KUJINYOFOA MANYOYA

Image
Kasuku ni ndege wapendwao na watu wengi sana hasa maeneo ya mjini. Ndege huyu hupendwa kwa sababu ana kasumba ya kuwa na rangi nzuri za kuvutia, achilia mbali rangi lakini pia ndege huyu ana sauti ambayo huwa haichoshi masikioni mwa watu, pia ni kivutio cha wengi.  Lakini licha ya kuwa na sifa hizo, ndege huyu amekuwaa na hulka moja ya kujinyofoa manyoa. Hii nikutoka na sababu mbalimbalia ambazo nitazieleza hapa na njia za kujikinga ili kasuku wako asinyofoke manyoa.  Kwa kuanza tuangalie sababu za kunyofoka kwa manyoa hayo  1. Lishe duni, upweke na kukosa matunzo ya jumla  2. Kama atakuwa anatafuna kucha zako unapomshika  3. Viroboto au utitiri  4. Maambukizi ya bakteria au fangasi  5. Banda dogo sana  6. Lishe yenye vitamini A kwa wingi zaidi  Nini kifanyike ili kuzuia tabia hii ya kunyofoka kwa manyoya  1. Hakikisha ndege wako anapata mlo kamili, unaweza kununua chakula kwenye maduka au ukachanganya mwenyewe baada ya kupata utaalam, apate matunzo yote muhimu na pia asiwe mwenyewe ni...

FAHAMU UFUGAJI WA NYUKI

Image
Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.  Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.  Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihita...

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE MABWAWA

Image
katika makala hii tunazidi kufahamishana fursa zinazotuzunguka,ambazo kwa uthubutu wa mtu yeyote katika jamii yetu anaweza kuzichukulia hatua na kuzifanyia kazi.  Kutokana na mahitaji ya samaki duniani kuzidi kushamiri kwa sababu ya ongezeko la wingi wa watu na uhaba wa sehemu zenye maji ya asili kama mito na maziwa kwa samaki wa maji baridi pia bahari kwa samaki wa maji chumvi,kumezidi kuhamasisha watu kungundua namna za kuweza kujipatia kitoweo hichi haswa ikichochewa na hamasa inayotokana na faida ya nyama nyeupe ya samaki katika mwili na afya ya binadamu.  Ufugaji wa samaki kwenye mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani kote inchi kama Thailand, China, Indonesia, Peru n.k  Niwazi tumeona baadhi ya inchi nyingi zikizidi kuzalisha nafasi nyingi za ajira kwa shughuli hizi pamoja na kukuza kipato cha mhusika mmoja mmoja, jamii flani na taifa kwa ujumla.  Katika kuiangalia fursa hii tutaangalia vipengele ambavyo kwa kufatilia wataalamu na wafugaji mbali mbali tumegundua vitasaid...

TAMBUA MASHARTI YA NJIWA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUWAFUGA

Image
1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike).  2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka.  3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.  4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!.  5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi.  6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena.  7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja.  8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kams honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama.  9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unash...

UTAYATAMBUAJE MAYAI YANAYOFAA KUTOTOLESHA

Image
Vigezo vya uchaguzi wa mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kutotoleshwa Si kila yai linalotagwa na kuku basi linakidhi sifa na vigezo vya kutotoleshwa ni wazi kuwa kama yai halikidhi vigezo vya kutotoleshwa na kuwa kifaranga hata uwezekano wa kutototoleshwa wenyewe unakuwa haupo. Wafugaji wengi tumekuwa tukikusanya mayai hovyo hovyo na kuyapelekwa kutotoleshwa bila kuzingatia vigezo hivi muhimu;- 1. A) YAWE YAMERUTUBISHWA NA JOGOO Sifa kuu na muhimu ya utotoleshwaji wa mayai ni kuwa ni lazima yawe yamerutubishwa na jogoo kwa uwiano stahili wa majogoo na mitetea na uwiano unaopendekekzwa ni wa mitetea nane kwa jogoo mmoja. 2.YAWE NA GANDA SAFI LISILO NA UFA Mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kutotoleshwa ni lazima yawe na ganda safi lisilo na uchafu uliogandia.Usafi wa mayai unategemea pia na usafi wa bandani na mahali ambapo kuku wanatagia. Iwapo kuku watakua na miguu misafi na wanataga kwenye viota visafi na ukusanyaji wa mayai unafanywa kwa wakati na kuwekwa kwenye chombo kisafi ni wa...