Posts

Showing posts from September, 2020

KILIMO CHA KABICHI

Image
KILIMO CHA KABICHI  Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa(cauliflower),kibichi kichina na kale.  MIZIZI  mizizi ya kabichi hutawanyika ardhin vizuri kwa kawaida huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 CM) na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano(75CM)  SHINA  Shina La mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au Zambarau.Hii hutegemeana na aina ya kabichi na kwa kawaida ni fupi.  HALI YA HEWA  Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi.Joto Jingi pia husababisha kulegea kwa kichwa vilivyofunga.Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari  UDONGO  Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huwo usiwe na chumvi chumvi nying na usiotuamisha maji.Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo ...