Posts

KILIMO CHA MTAMA

Image
Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa . HALI YA HEWA IFAAYO Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali seheme zenye baridi.Huita...

FAHAMU KUHUSU MBUZI BORA WA NYAMA- BOER GOAT

Image
ASILI Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka bara Ulaya na India , hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama. RANGI Wana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi  (brown)  ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001% UMBO Wana umbo kubwa kufikia kilo  110-135 kwa madume Kilo  90-100  kwa majike Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi  (Nubians) UZAZI Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi  (docile) Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba *Kama unamakala yako maalumu unataka tuiweke hum...

UFUGAJI BORA WA SUNGURA

UTANGULIZI Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu MABANDA Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura. UFUGAJI WA NDANI 1 – Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha 2 – Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuis...

FURSA KWENYE KILIMO CHA MUHOGO

Image
      Habari za leo mjasiriamali wa Kilimo. Leo napenda kukuletea somo kuhusu kilimo cha  Muhogo . Kama kawaida kazi yangu kubwa ni kuhakikisha unafanikiwa kwenye eneo la kilimo, kwa kukuletea elimu sahihi na fursa mbalimbali zinazohisiana na Kilimo. Wiki iliyopita tuliangazia kwa kifupi fursa ya kilimo cha Papai. Leo nitapenda tuangazie fursa ya kilimo cha Mihogo. Je wajua China na Tanzania zimesaini Mkataba wa Soko la Mihogo? Kama hufamu basi nikuelezee kwa ufupi. Ni hivi, Nchi ya China ni moja ya nchi zinazotumia sana zao la  muhogo.  China imeingia mkataba na Serikali ya Tanzania wa soko la mihogo, ambapo Tanzania itapaswa kuuza China mhogo Tani laki moja (100,000) kwa mwaka. Hata hivyo toka mkataba huo usainiwe hadi leo mwaka mmoja tayari umepita. Ila kwa mwaka wa kwanza, Tanzania tulifanikiwa kuuza tani 10,000 pekee (sawa na asilimi 10% tu ya kiasi kinachohitajika). Hivi karibuni nilimsikia Balazi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akisema, licha ...

KILIMO BORA CHA MPUNGA

Image
Maandalizi sahihi ya shamba  ni jambo la msingi katika  kuboresha kilimo cha umwagiliaji  wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu  bora zinazoshauriwa kutoonyesha  matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji.  Kimsingi maandalizi ya shamba  yanatakiwa yafanyike kwa usahihi na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga 1. KUSAFISHA SHAMBA Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji. 2. KULIMA Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na kuchanganya mas...