Posts

Showing posts from November, 2019

KILIMO CHA MTAMA

Image
Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa . HALI YA HEWA IFAAYO Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali seheme zenye baridi.Huita...

FAHAMU KUHUSU MBUZI BORA WA NYAMA- BOER GOAT

Image
ASILI Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka bara Ulaya na India , hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama. RANGI Wana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi  (brown)  ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001% UMBO Wana umbo kubwa kufikia kilo  110-135 kwa madume Kilo  90-100  kwa majike Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi  (Nubians) UZAZI Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi  (docile) Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba *Kama unamakala yako maalumu unataka tuiweke hum...