KILIMO CHA VIAZI VITAMU
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao y ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma. Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji. Aina za viazi vitamu Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista. Faida: vina wanga, vitamin, kambalishe, madini ya kalisiuamu, potasiamu, chuma, protini, na kal...